Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa al-Wala'i, Katibu Mkuu wa vikosi vya “Sayyid al-Shuhada”, ameusifu uwezo mkubwa na thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akautaja kuwa mstari wa mbele miongoni mwa nchi kubwa kutokana na uthabiti wake na irada yake katika makabiliano ya hivi karibuni.
Al-Wala’i katika taarifa yake siku ya Jumatano alisema kuwa; dunia ya leo inashuhudia “kuibuka kwa nguvu kubwa”, ambayo ni Iran, na akaamini kuwa ushindi wa hakika uko kwa wapiganaji wa “mhimili wa muqawama”, kutokana na imani yao kamili na kujisalimisha kwao.
Al-Wala’i, kwa kutumia lugha ya ishara na ya kidini, alielezea hali ya uwanja wa mapambano na kusema: “Wanajeshi wa Ali kwa mara nyingine wanavunja kuta za Khaybar”, na akaona kukubaliwa kuanza kwa mazungumzo kwa masharti ya Tehran kuwa ni ishara ya kuvunjika kwa “ubabe wa Nimrud”.
Katibu Mkuu wa vikosi vya “Sayyid al-Shuhada” katika hotuba yake pia alieleza kwamba Donald Trump, Rais wa Marekani, amelazimika kukubali masharti ya Iran, na akamwelezea kuwa ameshindwa mbele ya uthabiti na azma ya Tehran pamoja na washirika wake katika eneo hilo.
Maoni yako